Home » » KATA YA KWADELO WAZIDI KUJIKITA KATIKA KILIMO KWANZA

KATA YA KWADELO WAZIDI KUJIKITA KATIKA KILIMO KWANZA

 Diwani Kata ya Kwadelo Kondoa mkoani Dodoma Alhaji Omar Kariati
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya wakulima wa kata
hiyo kukabidhiwa matrekta mannem kwenye Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es
Salaam, leo. Julai 26, 2012.
 Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo za
trekta, mkulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani,  katika hafla ya
diwani huyo kukabidhi matrekta manne wakulima kutoka kata hiyo, kwenye
Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT,
Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao
kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana
kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja  ambayo
inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu
ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki katika kipindi cha miaka minne
kwa udhamini wa diwani huyo. Wengine, ni wakulima wa kata hiyo ya
Kwadelo,  Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (wapili kushoto) na Meneja wa
Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix  Samillan.
  Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix  Samillan akisalimiana
na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omar Kariati wakati
wa hafla ya wakulima wa kata hiyo kukabidhiwa matrekta mannem kwenye
Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es Salaam, leo. Julai 26, 2012.
 Mkulima wa Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Gaberiel Galahenga
akimkabidhi barua Diwani wa Kata hiyo,  Omari Kariatikwa ajili ya diwani
huyo kumpelekea kama shukurani Mkuu wa JKT, kwa shirika la Suma JKT
kuwawezesha wakulima wa kata hiyo kukubali kuwapa mattekta wakulima wa
kata hiyo kwa nusu ya bei na kisha kumalizia pole pole. Wengine katika
picha ni,   Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (watatu kushoto) na Meneja
wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix  Samillan.

Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto)
akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani
(kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta
manne, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012.
Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina
trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani
Kariati. Trekta moja  ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao
wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki
katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa