Masoud Masasi, Dodoma Yetu
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wameaswa kutochagua kiongozi kwa kuangalia kabila ama dini na badala yake wachague kiongozi atayekisaidia Chama.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma mjini ndugu Dennis Bendera ameeleza hayo katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi UVCCM uliofanyika juzi katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Amesema Kama mgombea anasimama na kuhubiri Dini ama Kabila Huyo hafai kuwa kiongozi bora takayekipeleka Chama mbele.
"Ukiona kiongozi au mgombea anazungumzia udini ujue amefilisika, wanachama hawahitaji dini ya mtu wala Kabila Bali wanahitaji kiongozi bora"Alisema Bendera.
Katika Uchaguzi huo ndugu Shabani Bwanga ameshinda nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM katika wilaya hiyo baada ya kupata kura 260 dhidi ya wapinzani wake Ndugu Maua Hassan aliyepata kura 87 na ndugu Juma Motoro aliyepata kura 79.
Walioshinda wengine ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Ccm wilaya ameshinda Ahmed Kibamba kwa kura 164 huku mkutano mkuu wa Uvccm Taifa waliopita ni zakaria Manyika kwa kura 311 na selemani serera kwa kura 241.
Mkutano mkuu UVCCM Mkoa nafasi 5 ambao ni Caroline Malecela, Erick Ngwega, Hamisa Kikwega,Rozi Michael na Shaban Shaban.
Baraza la Uvccm Mkoa Ally Barongo, Ahmad Kibamba Latifa Tawaqal na Baraza la Uvccm wilaya waliopita ni ahmed Kibamba, Fatuma Juma, Maua Hassani, Zuberi Zuberi, Rukia Mallya wakati nafasi ya ujumbe wa kuwakilisha wazazi ni Raymond Magoda na mjumbe wa kuwakilisha UWT Navrozi Murji.

Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment