Home » » MBUNGE BADWEL ASEMA KESI YAKE INA ‘MKONO’ WA TAKUKURU

MBUNGE BADWEL ASEMA KESI YAKE INA ‘MKONO’ WA TAKUKURU


Mbunge wa jimbo la Bahi Omar Badwel amesema kesi yake ya rushwa inayo mkabiri imetengenezwa kwa lengo la kumuua kisiasa,amesema njama hizo zimepangwa na wanasiasa na Takukuru Makao makuuu
Alisema kama kweli angekua amekula rushwa Chama chake CCM kingechukua hatua kali juu yake lakini kwa kuwa hata CCM imegundua ni uzushi ndio maana yupo salama na anaendelea kuwa Mbunge.
“Wananchi msiwe na wasiwasi mimi ni mbunge wenu na nitaendelea kuwa Mbunge wenu haya mnayo yaona ni uzushi tu wa wanasiasa na hao wanao jiita Takukuru" kauli hizo alizitoa katika kijiji cha Chibelela na Mwitikila Jimboni Bahi Mkoani Dodoma,
Akiwa Mwitikila alito laki tano kwa kikundi cha washonaji nguo na kuwambia kuwa waendelee kumuombea ashinde kesi yake na wafitini wote waumbuke!
Chanzo: Jamiiforum

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa