350,000 katika benki zake zilizopo hapa nchini jambo ambalo wamesema
likifanya kushindwa kusambaza damu ya kutosha katika hospitali
mbalimbali.
Hayo yalibainishwa na Meneja wa Mpango wa DamuSalama kanda ya
Mashariki Grace Mlingi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari mjini Dodoma juu ya mwamko wa wananchi katika kujitolea damu
katika benki za damu hapa nchini.
Mlingi amesema hatua hiyo ya kutokuwa na damu ya kutosha hapa nchini
inatokana na kutokuwa na mbadala wa upatikaji wa damu salamuisipokuwa
kutoka kwa binadamu.
Amesema wananchi wengi wamekuwa wakishindwa kujitokeza kwenye sehemya
utoleaji damu zaidi ya kuwapata wanafunzi peke yake jambo alilosema
halipendezi kwa kuwa damu hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya watu wote.
Meneja huyo alibainisha kuwa kuchangia damu kunasaidia kuepusha vifo
kwa watoto wadogo,wajawazito pamoja na majeruhi ambao wamekuwa
wakihitaji damu kutokana na kuishiwa hivyo kuwepo kwa damu za kutosha
kutachangia kuepukana na tatizo hilo.
Akizungumzia mahitaji ya damu katika kanda ya Mashariki,Mlingi amesema
wanahitaji chupa za damu 80,000 sawa na asilimia 67 ili ziweze
kukidhi mahitaji ya kanda hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Umma na Uhamasishaji wa mpango huo
katika kanda hiyo Lucas Michael alisema bado elimu kubwa inahitaji
kwa wananchi juu ya suala nzima la uchangiaji wa damu salama.
Amesema wananchi wamekuwa na imani potofu kuwa ukitoa damu unaweza
kupoteza maisha huku wengine wakiohofu kuwa watapimwa ukimwi kabla ya
kutoa damu.
0 comments:
Post a Comment