Home » » wakulima alizeti wasema kuongezwa kwa kodi kwa mafuta yanayoingizwa kutoka nje itasaidia kuwepo kwa soko la uhakika‏

wakulima alizeti wasema kuongezwa kwa kodi kwa mafuta yanayoingizwa kutoka nje itasaidia kuwepo kwa soko la uhakika‏


Masoud Masasi- Dodoma yetu Blog
BAADHI ya wakulima wa zao la Alizeti wamesema kitendo cha kuongeza kwa
kodi ya mafuta ya kupikia yanayoingizwa kutoka nje ya nchi kutawafanya
zao hilo sasa kuweza kupanuka kibiashara.
Walisema serikali imeweza kusikia kilio cha cha siku nyingi kwani
mafuta hayo yalikuwa yakiingizwa chini kwa kodi ndogo jambo
linalofanya kuuza kwa bei ya chini ikilinganishwa na mafuta ya
alizeti.
Hayo yalibainishwa jana mjini Dodoma na wakulima wa zao la Alizeti
wakati wa warsha ya siku ya mbili ya wakulima ambao ni wadau taasisi
ya Rural Livelihood Development Company(RLDC)inayojihusisha na
shughuli za kilimo na ufugaji.
Wakulima hao wamesema moja ya changamoto kubwa waliyokuwa wanakutana
nayo ni soko la mafuta ya alizeti kuwa dogo kutokana na mafuta mengine
yanayoingizwa nchini kuuzwa kwa bei nafuu.
Rosemarina Jima mkulima wa zao hilo kutoka mkoani Singida amesema kwa
sasa wataweza kushindana katika soko la mafuta ya alizeti na mafuta
mengine kutokana na uongezeko la kodi kwa mafuta hayo yanayotoka nje
ya nchi.
Amesema kwa kawaida mafuta ya alizeti yalikuwa juu sana kwenye soko
lake ikilinganishwa na mafuta na hayo ambayo kwenye soko lake yalikuwa
yakiuzwa kwa bei ya chini hatua iliyofanya mafuta ya alizeti kutouzika
kwa kiwango kikubwa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa