Home » » VIZIWI WALIA KUBAGULIWA KATIKA FURSA YA KUPATIWA AJIRA NCHINI.‏

VIZIWI WALIA KUBAGULIWA KATIKA FURSA YA KUPATIWA AJIRA NCHINI.‏


Mwandishi wetu- Dodoma yetu Blog
CHAMA cha Viziwi Tanzania(CHAVITA)kimelalamikia hatua ya baadhi ya
waajiri nchini kuwabagua walemavu katika suala la kuwapatia ajira
mbalimbali huku wakiwa na sifa za kuweza kupata ajira hizo lakini
wamekuwa hawapati fursa hiyo.
Sambamba na hilo pia walemavu hao wamesema wamekuwa na changamoto
katika huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya kutokana na kukosa
kwa mawasiliano ya uhakika baina yao na watoa huduma hao.
Hayo yalibainishwa na makamu mwenyekiti wa CHAVITA Melise Swila
wakati wa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
wao wanavyobaguliwa katika fursa ya kupatiwa ajira hapa nchini.
Swila amesema jamii ya viziwi na walemavu wengine wamekuwa na
changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira kutokana na wao kutopewa
kipaumbele katika kupatiwa ajira mbalimbali hapa nchini hatua
aliyosema ushirikishwaji umekuwa mdogo sana kwao katika jamii.
Amesema viziwi wengi hapa nchini hawana ajira yoyote hatua inayofanya
kuwazidishia umasikini uliotopea na kuonekana mzigo kwa taifa.
Akizungumzia suala la elimu na huduma ya afya amesema elimu ya viziwi
nchini inasikitisha kutokana na kukosekana kwa walimu wenye ujuzi wa
kutumia lugha ya alama na kubuni nyezo za kufundishia na kujifunzia
kwa viziwi.
Swila amesema kwa upande wa huduma za afya hali si nzuri kwa jamii ya
viziwi kutokana na kukosa huduma stahiki ambapo amesema hiyo
inasababishwa na kukosa kwa mawasiliano baina yao na madaktari pamoja
na wahusika wengine wa vituo vya afya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa