Home » » DUWASA YAOMBA NGUVU NAIBU WAZIRI KUDAI MAMILIONI WANAYOZIDAI TAASISI ZA KIJESHI‏

DUWASA YAOMBA NGUVU NAIBU WAZIRI KUDAI MAMILIONI WANAYOZIDAI TAASISI ZA KIJESHI‏


Masoud Masasi,Dodoma yetu Blog
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka mjini Dodoma(DUWASA)imemwomba Naibu wa
Waziri wa Maji kuwasaidia nguvu ili kuweza kulipwa kwa malimbikizo ya
Ankara ya maji ya sh 225.6 milioni wanazodai kwa taasisi za kijeshi
mkoani hapa pamoja na hospitali ya mkoa.
Taasisi hizo ambazo zinadaiwa kwa muda mrefu kutokana na kuwa wadaiwa
sugu ni jeshi la Polisi,Magereza na Jeshi la Kujenga taifa pamoja na
hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza wakati wa ziara ya Naibu waziri kwenye mamlaka hiyo
Binilith Mahenge,kaimu mkurugenzi wa Duwasa Sebastian Warioba amesema
taasisi hizo zimekuwa wadaiwa sugu kwa kipindi cha miezi sita.
Warioba amesema katika malimbikizo hayo jeshi la Polisi mkoani Dodoma
linadaiwa sh 95.2 milioni,jeshi la Magereza sh 47.5 huku jeshi la
Kujenga Taifa(JKT)lenyewe likidaiwa sh 51.3 ambapo amesema hospitali
ya mkoa yenyewe ikiwa inadaiwa sh 31.6 milioni madeni hayo yakiishia
juni 2012.
Amesema pamoja na kuwapa taarifa kuhusu madeni hayo lakini bado
hawajalipwa kiasi chochote cha pesa ambapo alimwomba naibu waziri
kuwasaidia ili kuweza kupatiwa fedha hizo.
Warioba amezitaja baadhi ya taasisi ikiwemo Ikulu,Bunge,Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM) kuwa zinaongoza kwa ulipaji mzuri wa Ankara ya maji
kwa mkoa.
Akizungumzia suala hilo naibu waziri Mahenge alisema atalishughulikia
suala hilo kwa kuzungumza na waziri husika ili kuona deni hilo
linalipwa ambapo pia aliwataka wasikatie maji taasisi hizo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa