Home » » CHAMA CHA SOKA DODOMA MJINI CHALIA NA PESA ZA KUENDESHEA LIGI YA WILAYA HIYO‏

CHAMA CHA SOKA DODOMA MJINI CHALIA NA PESA ZA KUENDESHEA LIGI YA WILAYA HIYO‏


Masoud Masasi,Dodoma yetu blog
CHAMA cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Dodoma Mjini(DUFA)kimesema
kinakabiliwa na ukata wa fedha za kuendeshea ligi ya wilaya
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza na Mwananchi Katibu wa chama hicho Said Mohamedi alisema
mpaka sasa chama hicho kinahitaji sh 4,727,000 kwa ajili ya kuendeshea
ligi hiyo.
Alisema fedha hizo zinatokana na gharama za kuwalipa waamuzi,posho za
kamisaa na wasimamizi,huduma ya kwanza,matengenezo ya uwanja pamoja na
zawadi za washindi.
Mohamedi alisema wanategemea kupata sh 2,450,000 ambazo ni kwa ajili
ya ada ya ushiriki wa ligi kwa timu 20 pamoja na viingilio vya
uwanjani katika hatua ya sita bora jambo alilosema msaada unahitajika
kwa wadau kuweza kukisaidia chama hicho.
“Tunakabiliwa na ukata wa fedha za kuendeshea ligi yetu ya wilaya
ambayo inaanza mwezi huu tunawaomba wadau wa soka mkoani hapa
kujitokeza kusaidia soka la dodoma kwa misaada mbalimbali”alisema
Babuji.
Katika hatua nyingine katibu huyo alisema jumla ya timu 22
zimeshachukuwa fomu za ushiriki ambapo amesema mwisho wa kurudisha ni
September 10 mwezi huu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa