Masoud Masasi,Dodoma yetu BlogWAAMUZI wa mchezo wa mpira wa miguu wamezitaka vyama vya mchezo huohapa nchini kuwepo kwa utaratibu wa kupatiwa mgao wa faini ambazowanazotozwa timu na wachezaji pindi mwamuzi anapojeruhiwa kwa kipigo.Hatua hiyo inatokana na waamuzi hao kudai kuwa wanaposhambuliwa nakujeruhiwa hakuna fungu lolote linalotoka kwa ajili ya matibabu zaidiya wao kujigharamia wenyewe huku faini hizo zikiingia ndani ya vyamahusika.Wakizungumza wakati wa kikao kati ya waamuzi wa mkoa wa Dodoma naMwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma(Dorefa)NasoroKipenzi,waamuzi hao walisema kuwepo kwa utaratibu wa wao kugaiwakifuta jasho kutokana na faini hizo.Mwamuzi Bam Bilasho alisema katika matukio hayo wakati mwingineujeruhiwa vibaya huku wakiibiwa vitu mbalimbali kutokana nakushambuliwa lakini inapotokea timu kutozwa faini pesa zote uingiandani ya chama husika huku wao wakijigharamia kila kitu kutokana nakupata majeraha.Bilasho alisema kuwepo na utaratibu kwa kamati za nidhamu za vyamambalimbali hapa nchini kuweka utaratibu wa kuwapa mgao wa pesazinazotokana na faini ambazo upewa mwamuzi aliyejeruhiwa.Mwamuzi mwingine Saleh Mang’ola alisema wao kama waamuzi huwa hawanabima yoyote jambo alilosema wanapopata matatizo uishia kutoa fedha zaomfukoni kujitibia jambo ambalo amesema wamekuwa wakibaguliwa sana.Mang’ola aliongezea kuwa wamekuwa wakilipwa posho ndogo wanapokwendakuchezesha mechi mbalimbali na wakati mwingine huwa wanakopwa jamboalilosema taaluma hiyo imekuwa haithaminiwi hapa nchini.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Dorefa Nassoro Kipenzi aliwataka waamuzihao kuwa makini wakati wanapochezesha mechi zao ili kuepukana na fujozinazoweza kufanya kujeruhiwa huku akiwahidi kuboresha posho kwawaamuzi wa mkoa huo kwenye mashindano yanayotambulika na chama hicho.
Home »
» WAAMUZI WA SOKA DODOMA WATAKA FAINI WANAZOTOZWA TIMU KWA AJILI YA KUPIGA WAAMUZI NAO WAPEWE MGAO
0 comments:
Post a Comment