Home » » chawata yaitaka serikali kuweka miundombnu rafiki kwa walemavu nchini‏

chawata yaitaka serikali kuweka miundombnu rafiki kwa walemavu nchini‏


Na Masoud Masasi Dodoma yetu
WALEMAVU nchini wameiomba serikali kuweka mkakati wa kujenga
miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa wao pia ni sehemu
ya jamii kama walivyo watu wengine.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa Chama cha watu wenye
ulemavu(CHAWATA)wilaya ya Dodoma mjini Kaleb Mhawi kwa niaba ya watu
wenye ulemavu wakati alipokuwa akizungumza na mkuu wa wilaya ya Dodoma
mjini Lephy Gembe wakati wa uzinduzi wa mradi wa uelewa wa sheria ya
watu wenye ulemavu ya mwaka 2010.
Mhawi ambaye pia ni mratibu wa mradi huo wenye thamani ya 44.5
milioni amesema watu wenye ulemavu wanachangamoto mbalimbali zikiwamo
za kijamii,kiuchumi,kisiasa na kisaikolojia.
Amesema changamoto kubwa wanayopata ni kutokuwepo kwa miundombinu
rafiki katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo kwenye
barabara,hospitalini na mashuleni jambo ambalo amesema limekuwa
likiwapa wakati mgumu.
Mhawi amesema katika majengo mengi ya serikali yamejengwa pasipo
kuwepo kwa miundombinu ambayo inaweza kumfanya mlemavu wowote kutoweza
kutumia.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Lephy Gembe aliwataka jamii hiyo
kuhakikisha inafanya kazi kulingana na haki zao za msingi na kuacha
kujinyanyapaa wenyewe kwani zipo kazi ambazo wanaweza kuzifanya pasipo
na shaka.
Amesema kwa upande wa miundombunu rafiki serikaliimeanza kulifanyia
kazi suala hilo kwa kuanza kujenga majengo ambayo yanasehemu ambayo
walemavu wanaweza kuyatumia pasipo na ugumu wowote.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa