Home » » WATANZANIA WATAKIWA KUEPUKNA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MABDILIKO YA TABIA NCHI‏

WATANZANIA WATAKIWA KUEPUKNA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MABDILIKO YA TABIA NCHI‏


Masoud Masasi,Dodoma
WANANCHI wametakiwa kudumisha hifadhi ya misitu,uoto wa asili na
uhifadhi wa mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya
hewa pamoja na tabia ya nchi.
Pia wametakiwa kudumisha kilimo mseto na uchanganyaji bora wa mazao
ya misitu,chakula na malisho ya mifugo kwa kutumia teknolojia rafiki
kwa mazingira ikiwa ni pamoja na miti yenye matumizi mazuri ya maji na
inayoruhusuukuaji wa mazao ya miti yenyewe.
Ushauri huo umetolewa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dodoma(UDOM)upande wa hifadhi ya Bailojia na Mazingira Dr Chrispinus
Rubanza wakati alipokuwa akitoa mada mabadiliko ya hali ya hewa na
tabia ya nchi na athari zake kwa maendeleo ya nchi iliyofanyika katika
tarafa ya Hombolo mkoani hapa.
Rubanza alisema kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kutochoma moto
miti,kulima kilimo cha mseto na kuepukana na kilimo cha kuhama hama
kutaweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Mabadiliko ya tabia ya nchi yanaweza kuepukika kwa kudumisha kilimo
cha mseto,kuzuia uharifu wa mazingira kwa kutochomo miti na kukata na
kuepukana na kilimo cha kuhamahama kutosaidia kukabiliana na mabadilo
haya”alisema Rubanza.
Alisema athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ni ukame unaotokana na
uhaba wa maji,ongezeko la wadudu wa mazao na waletao magonjwa ya
mazao,mifugo na wanyamapori hapa nchini.
Alibainisha kuwa hali itaweza kufanya kuwepo kwa upungufu wa akiba ya
chakula itakanayo na upunguaji wa uzalishaji wa mazao shambani.
“Mabadiliko haya kwa kiwango kikubwa yanasababishwa na ongezeko la
joto duniani inafanya kubadilika kwa mikondo ya mvua,kubadilika kwa
kina cha bahari kubadilika kwa muelekeo wa kasi ya upepo na kuongezeka
kwa uwezekanowa kutokea kwa maafa kama vile ukame,mafuriko na
kimbunga”alisema.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa