Masoud Masasi Dodoma Yetu Blog
DIWANI wa Kata ya Mlowa wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Aran Matewa (CCM) na wenzake wanne jana walifikishwa kizimbani katika Mahakama ya hakimu Mkazi wilaya ya Dodoma kwa kosa la mauaji yaliyotokea Agost 30 mwaka huu.
Diwani huyo na wenzake wanakabiliwa na kosa la kumuua Patrick Mwangatwa (43) akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Aidha diwani huyo jana hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na hivyo hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Verynice Kawiche, aliahirisha kesi hiyo hadi Octoba tisa mwaka huu.
Kawiche, hakuwatayari kusikiliza maelezo ya diwani huyo baada ya kunyoosha mkono na kuiambia mahakama kuwa wao hawahusiki na mauaji hayo.
Hatahivyo Diwani huyo na wenzake walipandishwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa Agosti 31 wakiwa Mlowa mahali ambapo mauaji hayo yalifanyika.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama kaka wa marehemu Andrew Mwangatwa, amesema kuwa mdogo wake aliuawa akiwa chini ya ulinzi wa polisi na mtu wa kwanza kuanza kumshambulia alikuwa ni diwani ambaye alianza kwa kumpiga na ubao.
Hatahivyo taarifa zinasema kuwa, siku ya tukio marehemu Patrick alikuwa kijijini kwake Makang’wa na ndipo alipokuja diwani Matewa akiwa amefuatana na polisi wawili na kumtaka marehemu aongozane nao hadi kituo cha Polisi Mvumi.
Safari hiyo ya Mvumi iliishia njiani baada ya diwani kumuarisha marehemu apelekwe kijiji jirani cha Mlowa na walipofika hapo, walimfunga pingu na kugonga kengere ya hatari ndipo wananchi walipofika na diwani akaamuru waanze kushambulia marehemu bila ya kueleza sababu huku yeye akianza kwa kumpiga na ubao.
Kwa mujibu wa ndugu wa maremu wanasema kuwa Patrick alikufa akiwa na pingu za polisi mikononi huku akiwa amelowa damu mwili mzima na majeraha likiwemo jeraha kubwa tumboni ambalo lilisababisha utumbo wake kumwagika nje.
0 comments:
Post a Comment