Masoud Masasi,Dodoma
MWAMUZI mkongwe wa mchezo wa soka nchini Idd Ngongite amewajia juu baadhi ya makocha na wachezaji wanaolalamikia waamuzi kutochezesha vizuri mechi na kusema kinachowasumbua ni kutojua vizuri sheria 17 za mchezo huo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwamuzi huyo mzoefu katika mchezo wa soka hapa nchini alisema kuwa makocha na wachezaji wengi wamekuwa hawajui vizuri sheria 17 za soka zilizoweka jambo linalofanya kuwepo kwa malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa makocha hao ambao hawajui sheria hizo.
Ngongite maarufu kama Kabambe alisema kuwa katika uzoefu wake wa mchezo wa soka makocha wengi pamoja na wachezaji wamekuwa hawajui kabisa sheria za mchezo huo hatua inayofanya kuwa walalamishi wakati wote wa mchezo.
“Mimi ni mwamuzi toka miaka ya sabini najua kabisa hawa makocha na wachezaji wengi hawajui kabisa sheria 17 za mchezo wa soka na ndio hao wanaoharibu mchezo wanawazonga waamuzi kwa jambo ambalo liko kwenye sheria za mchezo mwisho mwamuzi anapigwa”alisema Ngongite kwa masikitiko.
Alisema kuwa mara nyingi waamuzi wanakuwa wanachezesha mchezo ndani ya sheria hizo lakini cha ajabu makocha hao pamoja na wachezaji wao wamekuwa wakilalamika kutotendewa haki jambo linalomtia mashaka kwamba hawajui sheria za soka.
Mwamuzi huyo alisema sasa iko haja ya shirikisho la Soka nchini(TFF) kuwa wanatoa semina kwa makocha na wachezaji kabla ya ligi kuanza juu ya sheria 17 za mchezo wa soka ili kuondoa malalamiko ya waamuzi kuvurunda mechi.
Hata hivyo Ngongite aliwataka TFF kuboresha maslahi ya waamuzi ili kuzuia mihanya ya rushwa kutoka kwa timu mbalimbali zinazowarubuni.
“Unajua waamuzi ni sehemu kubwa sana ya mchezo lakini tukija katika suala la maslahi kwa kweli ni madogo sana na hii inafanya kuwa wepesi kurubuniwa na timu,lakini kama TFF wataboresha maslahi yao basi hawataweza kurubuniwa kabisa”alisema
Katika hatua nyingine mwamuzi huyo aliwataka waamuzi kuchezesha mchezo huo kwa kufuata sheria hiz o ili kuondokana na lawama hizo kwa kuwa wao ni sehemu ya kuleta maendeleo ya mchezo wa soka iwapo wakifuata sheria hizo.
Chanzo: www.blogszamikoa.blogspot.com
Chanzo: www.blogszamikoa.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment