Home » » NJAA KUIKUMBA WILAYA YA KONGWA

NJAA KUIKUMBA WILAYA YA KONGWA



Na Debora Sanja, Dodoma
ASILIMIA 20 hadi 30 za Kaya za Wilaya ya Kongwa, zipo hatarini kukumbwa na njaa katika kipindi cha mwaka 2012/2013. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kongwa, Athumani Akalama.

Alisema hali hiyo inatokana na ukame uliokumba wilaya hiyo katika kipindi cha Januari hadi Februari, mwaka huu.

“Ukame huo uliathiri mazao yaliyokuwa yakitarajiwa kukomaa mapema Aprili hadi Machi, ili yatumike kama chakula hasa kwa familia za kipato cha chini.

“Athari ya ukame ilitofautiana kwa maeneo na kwa mazao, kwa ujumla mazao karibu yote yaliathirika lakini kwa viwango tofauti.

“Zao lililoathirika zaidi ni mahindi kwa wastani wa asilimia 30, zao la mtama kwa asilimia tano, alizeti na mazao ya jamii ya mikunde yaliathiriwa kwa asilimia 15.

“Hivyo katika kipindi cha Machi, mwaka huu, upungufu wa chakula katika kaya zenye kipato cha chini utaongezeka,” alisema Akalama.

Alisema Wilaya ya Kongwa imekuwa ikiwahamasisha wananchi kuhifadhi chakula cha kutosha kwa mwaka mzima kulingana na mahitaji ya familia kwa kiwango cha gunia tatu za nafaka kwa mtu kwa mwaka.

“Kaya zenye upungufu zimehamasishwa kununua chakula wakati huu wa mavuno kwa kuuza mifugo au mazao ya biashara waliyoyavuna.

“Kila kaya inatakiwa kuhifadhi vizuri mavuno iliyoyavuna msimu huu na pia tumepiga marufuku matumizi mabaya ya chakula.

Chanzo: Mtanzania


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa