Home » » SERIKALI YATAKIWA KUWAWEZESHA WALEAMVU KUJUA SHERIA ZAO‏

SERIKALI YATAKIWA KUWAWEZESHA WALEAMVU KUJUA SHERIA ZAO‏


Na Masoud Masasi
SEPTEMBA 2012   WALEMAVU…
WITO umetolewa kwa Serikali  kuziwezesha jamii za watu wenye ulemavu nchini kuzitambua sheria zinazowahusu jamii hiyo ili waweze kuzitumia katika kudai haki zao za msingi na kuwa msaada mkubwa kwao kwa kuwa wengi bado hawazijui.

Kauli hiyo ilitolewa le na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Chamwino mkoani Dodoma Amani Msanga wakati alipokuwa akifungua warsha kuhusu sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 kwa watendaji na wadau wa halmashauri hiyo.

Msanga amesema serikali lazima iweke mikakati ya kuwasaidia watu wa jamii ya ulemavu katika kuilewa sheria hiyo ili iwe msaada kwao katika kusimamia haki zao za masingi.

Alibainisha kuwa katika sheria hiyo inaelekeza kuwa serikali kupitia halmashauri zinatakiwa kuwasaidia walemavu lakini zimekuwa hazina mafungu ya kutosha kwa ajili ya watu wenye ulemavu hapa nchini.

Amesema sera ya watu wenye ulemavu imekuwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo na usimamizi wa kutosha katika kujenga miundombinu rafiki kwa walemavu.
Pia alishauri kwenye wizara ya elimu iwe na naibu waziri anayehusika na walemavu pekee kwa kuwa takwimu zinaonyesha asilimia 10 nchini ni walemavu.
Kwa upande wake mratibu wa warsha hiyo, Omary Lubuva, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watu wenye ulemavu katika wilaya hiyo kuweza kutambua haki zao na kuweza kuzidai kila wanapozikosa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa