Home » » wachezaji 10 wawekewea pingamizi ligi wilaya ya dodoma mjini kwenye uchambuzi wa fomu za usajili‏

wachezaji 10 wawekewea pingamizi ligi wilaya ya dodoma mjini kwenye uchambuzi wa fomu za usajili‏


Masoud Masasi,Dodoma
JUMLA ya wachezaji 10 wamewekewa pingamizi wakati wa uchambuzi wa fomu za usajili wa ligi taifa ngazi ya Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kusajili zaidi ya timu moja.
Katibu wa Chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Dodoma Mjini(DUFA)Said Mohamed Babuji alisema wachezaji hao wamewekewa pingamizi na timu zao baada ya kuonekana wamesajiliwa na timu nyingine.
Babuji aliwataja wachezaji hao kuwa ni Abdulsaid Salehe,Ibrahimu Omari,Maximilian Victor walioekewa pingamizi na timu ya Dodoma Sports,Nasoro Hamduni(Area D)Hamisi Habibu na Adolf Mkuyu(Ac Hungry)Moroco Jeremia na Bakari Mohamed(Dundee United)Issa Mfaume na timu ya West Chinangali.
Katibu huyo alisema wanawapa wiki moja vilabu vilivyowekeana pingamizi kumalizana wao wenyewe kabla ya wao kuchukua hatua kali kwa wachezaji hao ambao amesema watawafungia kucheza mpira wa miguu wilayani hapa kama watashindwa kuafikiana kuhusu usajili huo.
“Sisi tunachotaka vilabu ambavyo wachezaji waliosajili wamewekewa pingamizi kukaa mezani kuafikiana ndani ya wiki moja baaa ya hapo sisi hatua itakayofuata tutaangalia kanuni zinasemaje basi tutachukua hatua stahiki kwa wachezaji hao”alisema Babuji.
Katika uchambuzi huo timu nne zilishindwa kuchambuliwa baada ya fomu zao kuonekana kuna mapungufu mbalimbali ikiwepo kutokuwepo wa picha,sahihi za wachezaji pamoja na muhuri wa timu zao kwenye fomu hizo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa