Masoud Masasi,Dodoma
TIMU ya Dodoma Sports itakayoshiriki ligi taifa ngazi ya Wilaya ya Dodoma Mjini imesema katika usajili wake imesajili wachezaji chipukizi katika kuhakikisha wanainua vipaji hivyo mkoani hapa na kuzitaka timu nyingine kutumia zaidi wachezaji hao badala ya wazee ambao wametakiwa sasa kushiriki kwenye mabonanza pekee.
Katibu mkuu wa timu hiyo Kassimu Chavai alisema katika usajili huo wa mwaka huu wamesajili wachezaji vijana waliochini ya umri wa miaka 15-19 ikiwa ni lengo la kunuia vipaji vyao ambavyo vimekuwa havionekani kutokana na kutopewa nafasi ya kucheza mpira wa miguu badala yake nafasi hizo zimekuwa wakicheza wazee ambao wamekuwa wakicheza chini ya kiwango kutokana na soka lao kuisha.
Chavai alisema kwa timu ya Dodoma Sports kwa sasa haitosajili wachezaji walio na umri mkubwa kwa kuwa wameona wakiendelea kufanya hivyo soka la mkoa huo alitaweza kusonga mbele.
“Timu yetu msimu huu hakuna mzee pale tumesajili vijana wadogo kabisa hawa wazee wakacheze kwenye mabonanza na si kwenye ligi hizi nah ii itasaidia sasa kukuza vipaji vya hawa watoto wetu kwa kuwapa nafasi ya kucheza”alisema Chavai.
Kwa upande wao akizungumza hivi karibuni wakati wa zoezi la uchambuzi wa fomu kwa vilabu vya wilaya hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Dodoma(DUFA)Juma Kikanya alivitaka vilabau hivyo kuwatumia zaidi vijana ambao wamekuwa wakikosa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye ligi mbalimbali mjini hapa.
“Tuwatumie zaidi vijana kwenye ligi yetu itakayoanza kwa kua tukifanya hivi tutaweza kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wetu wa Dodoma kwa kuweza kuwapa nafasi hawa vijana ”alisema Kikanya.
Chanzo: www.blogszamikoa.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment