Home » » WAFUGAJI MPWAPWA WAFIKIRIA KUACHANA NA UFUGAJI KUTOKANA NA KUKOSA MAENEO YA MALISHO

WAFUGAJI MPWAPWA WAFIKIRIA KUACHANA NA UFUGAJI KUTOKANA NA KUKOSA MAENEO YA MALISHO

Masoud Masasi, Dodoma Yetu
WAFUGAJI Wilayani Mpwapwa wamesema moja ya changamoto wanayoipata ni kukosekana kwa maeneo ya malisho ya mifugo hapa nchini kwa kuwa  sehemu hizo kutumika kwa shughuli za kilimo  jambo linalofanya wengi wao kuamua kuachana na ufugaji kutokana na wanyama kufa kwa njaa.

Pia wameitaka serikali kuhakikisha inatenga maeneo maalumu kwa ajili ya malisho ya mifugo ambapo wamesema hii itasaidia kuondoa migogoro kati yao na wakulima kutokana na mifugo yao kuingia mashambani.

Wamesema hatua hiyo inatokana na wakulima wengi kutumia ardhi kwa ajili ya shughuli hizo jambo linalofanya  kukosekana kwa kiasi kikubwa ardhi kwa ajili ya malisho.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti baadhi ya wafugaji katika kata ya Massa walisema  kutokuwepo kwa maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo kumechangia  kufa kwa wanyama jambo ambalo wamesema
linafanya wengi wao kuamua kuachana na ufugaji.

Pia waliitaka serikali kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya shughuli za ufugaji ili kuweza kuondokana na migogoro kati yao na wakulima ambayo wakati mwingine usababisha kutokuwepo kwa amani nchini.

Walibainisha kuwa maeneo mengi hapa nchini yamekuwa yakitengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo pekee jambo wamesema wao kukosa maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.

Katika hatua nyingine wafugaji hao wamesema kutokuwepo kwa maafisa wa mifugo wa kutosha katika maeneo yao ni moja ya changamoto wanayokutana nayo.

Wafugaji hao wamesema wengi wao hawana utaalamu wa mifugo hiyo jambo linalochangia mifugo kufa kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo wamekuwa wakishindwa kuyatambua.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa