Masoud Masasi, Dodoma Yetu
IMEFAHAMIKA kuwa kuwepo kwa bidhaa za ngozi zenye bei nafuu na zisizo na ubora zinazotoka nje ya nchi ndiko kunakochangia bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini kukosa soko la uhakika kutokana na watu wengi kununua bidhaa hizo kwa bei nafuu.
Hayo yalibainishwa na mwenyekiti wa kikundi cha utengenezaji wa bidhaa za ngozi cha kizota mjini Dodoma,Emmanuel Kibinda wakati alipokuwa akizungumzia soko la bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini.
Kibinda amesema kuwa uingizaji wa bidhaa za ngozi zinazotoka nje ya nchi ambazo uuzwa kwa bei nafuu ndiko kunakofanya wao kutoweza kuuza bidhaa zao kutokana na wao kuuza bidhaa hizo kwa bei ya juu kulingana na ubora wa bidhaa hizo.
Amesema wao wamekuwa wakitengeneza viatu,mikanda,mifuko ya kuhifadhia fedha,ambapo wamekuwa wakitengeneza bidhaa hizo kwa kutumia ngozi asilia wanazozalisha wenyewe katika kituo chao jambo linalofanya kuuza kwa bei tofauti na bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo amesema bidhaa za nje zimekuwa zikitengenezwa chini ya kiwango jambo linalofanywa bidhaa hizo kuuzwa kwa bei ya chini hatua inayofanya wengi kukimbilia kununua bidhaa hizo kutokana na bei yake.
Alitoa wito kwa watanzania kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwa kuwa ni bora kuliko zile zinazoagizwa nje ya nchi ambazo hazina ubora.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment