Home » » MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAATHIRI SHUGHULI ZA UTAFITI KTK KITUO CHA TAIFA CHA UTAFITI WA MIFUGO

MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAATHIRI SHUGHULI ZA UTAFITI KTK KITUO CHA TAIFA CHA UTAFITI WA MIFUGO

Masoud Masasi, Dodoma Yetu
TAASISI ya Taifa ya utafiti wa taifa ya mifugo(TALIRI) imesema mabadiliko ya tabia ya nchi yameathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za utafiti pamoja na uzalishaji katika kituo hicho.
Hayo yalibainishwa juzi mjini Dodoma  na mkurugenzi wa taasisi hiyo Dk David Sendalo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya changamoto zinazoikumba kituo hicho cha taifa cha utafiti.

Sendalo amesema kipindi cha nyuma shughuli za uzalishaji  na utafiti zilikuwa kwa ufanisi mkubwa kuliko ilivyo sasa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa taasisi hiyo.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa mabadiliko hayo ya hali ya hewa yaliyoathiri shughuli hizo yalitokana na upatikanaji mdogo wa mvua ambao hauzingatii misimu ya mvua jambo ambalo amesema ni kikwazo
kikubwa kwao.

Amesema jambo hilo limefanya mifugo kushambuliwa na magonjwa na kusababisha kufa  tofauti na kipindi cha nyuma ambacho kilikuwa na hali nzuri ya hewa na kusababisha uzalishaji kuwa na ubora.

Mkurugenzi huyo aliyataja  changamoto nyingine ni magonjwa ambayo yamekuwa tishio kwa mifugo hivi sasa kuwa ni pamoja na ugonjwa wa Lifty valley ambao  ulipoteza ngo’mbe wengi sana na ugonjwa wa mapafu ambao umejitokeza hivi sasa kuathiri  wanyama wadogo wakiwemo mbuzi.

Dk Sindalo amesema pia elimu inahitajika kwa wafugaji kwa kuwa wamebaini wengi wao hawana mafunzo ya kuweza kufanya shughuli hizo jambo alilosema linasabisha mifugo kutokuwa na afya bora na mingi kufa kutokana na magonjwa.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa