Masoud Masasi, Dodoma Yetu
CHAMA cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu(FRAT)mkoa wa Dodoma kimepata viongozi wapya watakaokitumikia chama hicho kwa kipindi cha miaka minne.
Akitangaza matokeo hayo juzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji wa kura katibu wa Kamati ya Uchaguzi wa chama hicho Goderiver Mnubi alisema katika uchaguzi huo jumla ya wapigakura 16 walishiriki uchaguzi huo.
Mnubi alisema nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho iko wazi baada ya mgombea Patrick Masumbuko aliyekuwa mgombea pekee kupigiwa kura za hapana 12 huku za ndio zikiwa ni tatu jambo kukosa sifa ya kuwa mshindi.
Kwa upande wa nafasi ya makamu mwenyekiti ilikwenda Laulent Chacha aliyepigiwa kura zote 16 za ndio ambapo nafasi ya Katibu ilichukuliwa na Samson Mkotya.
Mnubi alisema kwa upande wa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu imekwenda kwa Simon Charles huku nafasi ya mjumbewa kamati ya utendaji ikienda kwa John Charles.
Katika uchaguzi huo nafasi ya mweka hazina na mjumbe mwakilishi wa wanawake katika chama hicho ziko wazi baada ya kutojitokeza kwa wanachama kwa ajili ya kugombea.
Mgeni rasmi katika uchaguzi huo Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Miguu mkoa wa Dodoma (DOREFA) Nassoro Kipenzi aliwataka viongozi hao kujenga mshikamano ili kuweza kukifanya chama hicho kusonga mbele.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment