Masoud Masasi, Dodoma Yetu
WADAU wa mchezo wa Soka mkoani Dodoma wamezitaka vilabu vitakavyoshiriki ligi taifa ngazi za wilaya na mkoa hapa nchini kuwatumia zaidi vijana badala ya wazee kwa kuwa kufanya hivyo kutaweza
kuibua vipaji vyao na kuendeleza mchezo huo.
Walisema jukumu la kuibua vipaji vya vijana si mpaka mashindano ya Copa cocacola bali hata hizi ligi za chini zinaweza kuibua vipaji hivyo kwa kuwatumia katika timu zao na kuacha kasumba ya kuwatumia
wazee ambao mpira umeisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao ambao ni Bakari Bangu mchezaji wa zamani wa timu ya Dodoma Sports,Salum Ndambwe meneja wa zamani wa uwanja wa jamhuri pamoja kasimu Chavai kocha wa Dodoma Sports.
Walisema kamwe soka la Tanzania halitoendelea kama hawataweza kuwaandaa vijana katika ligi za chini ambazo ni sehemu ya vijana hao kuonyesha vipaji vyao katika mchezo huo ambavyo vimekuwa havionekani kutokana na kutopewa nafasi.
Wadau hao walisema timu nyingi hapa nchini zimekuwa zikiwatumia zaidi wachezaji ambao ni wazee katika ligi ngazi za wilaya jambo linalowanyima nafasi vijana kuonyesha kuonyesha vipaji vyao.
“Tukitaka soka letu liweze kuendelea lazima tuanze kuwatumia vijana katika ligi zetu za chini hasa hii ligi taifa ngazi za wilaya tuwatumie jamani kuliko kuwaacha na kuwatumia wazee ambao wamekwisa kwa sababu ya kuwa ni wakongwe tusisubiri hadi mashindano ya copa cocacola ili vijana wacheze”alisema Ndambwe mchezaji wa zamani wa Dodoma sports.
Waliongezea kuwa nchi za ulaya zinapata mafanikio kutokana na kuwatumia zaidi vijana katika ligi zao kuliko wazee jambo linalofanya soka lao kuwa na mvuto zaidi hivyo kama Tanzania itaweza kufanya hivyo mchezo huo utakuwa na mafanikio.
“Lakini mimi napenda kuwapongeza TFF kwa kweli wamefanikio kwa kiasi Fulani kuinua soka la vijana tofauti na kipindi cha nyuma wamekuwa wakianzisha program mbalimbali za kuinua na kuibua vipaji vya soka kupitia cocacola”alisema Ndambwe meneja wa zamani uwanja jamhuri Dodoma.
Ligi Taifa ngazi za wilaya zinatarajiwa kuanza kucheza katika wilaya tofauti hapa nchini ambapo mabingwa watawakilisha wilaya zao katika mashindano ya mkoa ba baadae kuwakilisha mikoa yao katika ligi taifa ngazi za mikoa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment