na Danson Kaijage, Kibaigwa
UMOJA
wa wakulima wa Kibaigwa katika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma na wakulima wa
Kiteto mkoani Manyara wamelazimika kumwandikia barua Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kumwomba aingilie kati mgogoro kati yao na wafugaji katika wilaya hizo.
Wakulima
hao wamechukua hatua hiyo ya kumwandikia barua Pinda kutokana na kulazimishwa
na uongozi wa wilaya ya Kiteto wasiendelee kulima mahindi katika mashamba yao
kwa madai kuwa ni maeneo ya wazi.
Barua
hiyo iliyoandikwa Agosti 15, mwaka huu, inamwomba Waziri Mkuu aingilie kati
mgogoro huo jambo linalosababisha uongozi wa mkoa wa Manyara kuwalazimisha
wakulima kusitisha shughuli zao za kilimo cha kila siku.
Kwa
mujibu ya barua hiyo, iwapo wakulima hawataruhusiwa kuendelea na kilimo katika
mashamba yao, ni wazi kuwa watajikuta wakipelekwa jela kwa ajili ya kushindwa
kurejesha mkopo wa trekta waliokopa hivi karibuni.
Hata
hivyo walisema kuzuiliwa kuendelea na kilimo huku mashamba yao yakitumiwa na
wafugaji kunaweza kuendeleza uhasama baina yao.
Mgogoro
kati ya wakulima na wafugaji umedumu kwa miaka saba sasa na kufikia hatua ya
watu kupoteza maisha kutokana na mapambano kati yao.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment