Home » » WANAWAKE WALIA KUBAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI HAPA NCHINI‏

WANAWAKE WALIA KUBAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI HAPA NCHINI‏

Masoud Masasi,Dodoma
WANAWAKE wamesema dhana ya usawa wa kijinsia hapa nchini hasa katika
nafasi za uongozi kwenye vyama vya siasa na serikali bado umekuwa
ukimbagua mwanamke katika kuumpa fursa ya kuongoza nafasi hizo licha
ya wao kuwa wengi katika idadi ya watu hapa nchini.
Hayo yalibainishwa na Katibu wa shirika lisilo la kiserikali
linaloshughulikia haki za wanawake la WOWAP Fortunata Makafu wakati
alipokuwa akiwasilisha mada katika mdahalo wa dhana ya usawa wa
jinsia kwa maendeleo ya jimbo la Dodoma mjini lilolofanyika mjini
hapa.
Makafu alisema kwenye vyama vya siasa hapa nchini nafasi zote za juu
za uongozi zimeshikiliwa na wanaume ambapo amesema hakuna hata chama
kimoja ambacho nafasi hizo zimeshikwa na mwanamke.
Alisema kwa upande wa serikali nafasi za mawaziri,makatibu wakuu na
wakurugenzi asilimia kubwa zimeshikwa na wanaume ambapo wanawake ni
wachache huku akisema idadi ya wanawake waliosoma ni kubwa lakini
wamekuwa wakibaguliwa katika kupata fursa hizo.
“Ukiangalia nafasi zote za juu katika uongozi wa vyama vya siasa hapa
nchini zimeshikwa na wanaume pekee kwa upande wa serikali baraza la
mawaziri wanawake wachache lakini wanawake ni wengi katika idadi ya
watu Tanzania lakini hawapatiwi fursa ya kutosha katika nafasi za
uongozi”alisema Makafu.
Alisema hatua hiyo inatokana na jamii kumwangalia mwanamke katika
jicho la kumuhukumu kuwa hawezi kuongoza hata kama ana uwezo mkubwa
kuliko mwanaume.
“Wakati mwingine jamii inakuwa inamukumu mwanamke kuwa hawezi kuongoza
hata kama ana uwezo mkubwa kuliko mwanaume lakini tumekuwa tuna uwezo
mkubwa katika nafasi chache tulizopewa na kuonyesha uchapa
kazi”alisema.
Alisema pia kwa upande wa ajira kazi na madaraka makubwa yenye
mishahara mikubwa hushikwa na wanaume huku wanawake wakiwa chache sana
waliopatiwa fursa hiyo hapa nchini.Masoud Masasi,Dodoma

waliopatiwa fursa hiyo hapa nchini.

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa