Home » » WANANCHI WATAKA KWENYE KATIBA MPYA KUWEKWE KWA SHARIA KALI KWA WANAOTEMBEA NUSU UCHI‏

WANANCHI WATAKA KWENYE KATIBA MPYA KUWEKWE KWA SHARIA KALI KWA WANAOTEMBEA NUSU UCHI‏


Masoud Masasi Dodoma yetu Blog
WANANCHI wa kijiji cha Hombolo mkoani Dodoma wameitaka katika katiba
mpya kuwepo kwa kipengele cha sheria ambacho kitamfunga zaidi ya mwaka
mwanaume au mwanamke atakayeonekana anatembea mitaani amevaa nusu
uchi.
Wakizungumza katika mdahalo wa kupata maoni ya katiba mpya
iliyoendelea katika vijiji vya Manispaa ya Dodoma,wananchi hao
wamesema sheria hiyo itaweza kukomesha vitendo vya wanaume kutembea
wamevaa chini ya makalio nguo zao na wale wanawake wanaovaa nguo
zinazoonyesha maungo yao ya mwilini.
Issa Ali mkazi wa kijiji hicho amesema jamii kwa sasa imekuwa katika
hali mbaya haswa kwa vijana kwa kuiga tamaduni za nje na kufanya kuvaa
nguo ambazo zimekuwa zikiwaacha uchi jamgo alilosema ni hatari kwa
vizazi vijavyo.
Juma Mohamedi amesema ili kuweza kukomesha tabia hiyo kuwepo kwa
sheria katika katiba mpya ambayo itakuwa ni kosa la jinai kwa mtu
kuonekana anatembea nusu uchi na kupewa adhabu kali ambayo kifungo
chake kisipungue mwaka mmoja.
Mkazi mwingine Yonadi Mtagwa amesema kama katika katiba mpya
kutawekwa kipengele hicho kutaweza kukomesha aibu iliyopo sasa ya
wanaume na wanawake kutembea nusu uchi kwa kuwa wengi wataogopa mkono
wa sheria.
Katika mdahalo huo wa kupata maoni ya wananchi juu ya nini kiwepo na
kitolewe kwenye katiba mpya zaidi ya wananchi 100 wa kijiji hicho
walishiriki katika mdahalo huo ulioandaliwa na mtandao wa asasi za
kiraia wa DUNGONET.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa