Masoud Masasi,Dodoma yetu blogWANAWAKE wamesema dhana ya usawa wa kijinsia hapa nchini hasa katikanafasi za uongozi kwenye vyama vya siasa na serikali bado umekuwaukimbagua mwanamke katika kuumpa fursa ya kuongoza nafasi hizo lichaya wao kuwa wengi katika idadi ya watu hapa nchini.Hayo yalibainishwa na Katibu wa shirika lisilo la kiserikalilinaloshughulikia haki za wanawake la WOWAP Fortunata Makafu wakatialipokuwa akiwasilisha mada katika mdahalo wa dhana ya usawa wajinsia kwa maendeleo ya jimbo la Dodoma mjini lilolofanyika mjinihapa.Makafu alisema kwenye vyama vya siasa hapa nchini nafasi zote za juuza uongozi zimeshikiliwa na wanaume ambapo amesema hakuna hata chamakimoja ambacho nafasi hizo zimeshikwa na mwanamke.Alisema kwa upande wa serikali nafasi za mawaziri,makatibu wakuu nawakurugenzi asilimia kubwa zimeshikwa na wanaume ambapo wanawake niwachache huku akisema idadi ya wanawake waliosoma ni kubwa lakiniwamekuwa wakibaguliwa katika kupata fursa hizo.“Ukiangalia nafasi zote za juu katika uongozi wa vyama vya siasa hapanchini zimeshikwa na wanaume pekee kwa upande wa serikali baraza lamawaziri wanawake wachache lakini wanawake ni wengi katika idadi yawatu Tanzania lakini hawapatiwi fursa ya kutosha katika nafasi zauongozi”alisema Makafu.Alisema hatua hiyo inatokana na jamii kumwangalia mwanamke katikajicho la kumuhukumu kuwa hawezi kuongoza hata kama ana uwezo mkubwakuliko mwanaume.“Wakati mwingine jamii inakuwa inamukumu mwanamke kuwa hawezi kuongozahata kama ana uwezo mkubwa kuliko mwanaume lakini tumekuwa tuna uwezomkubwa katika nafasi chache tulizopewa na kuonyesha uchapakazi”alisema.Alisema pia kwa upande wa ajira kazi na madaraka makubwa yenyemishahara mikubwa hushikwa na wanaume huku wanawake wakiwa chache sanawaliopatiwa fursa hiyo hapa nchini.
Home »
 » WANAWAKE WALIA KUBAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI HAPA NCHINI
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment