Home » » WATU 14 WAFARIKI KTIKA AJALI YA LORI KONDOA‏

WATU 14 WAFARIKI KTIKA AJALI YA LORI KONDOA‏


Na Masoud Masasi- Dodoma yetu Blog
WATU 14 WAMEKUFA NA WENGINE 73 KUERUHIWABAADA YA GARI WALIOKUWA
WAKISAFIRIA KUTOKA BEREKO KUELEKEA PAHI WILAYANI KONDOA MKOANI DODOMA
KUFUATIA YA LORI HILO KUACHA NJIA NA KUGONGA MWAMBA NA KUPINDUKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA ZELOTHE STEPHEN AMESEMA AJALI HIYO
IMETOKEA JANA MAJRA YA SAA TISA JIONI KATIKA KIJIJI CHA MNENIA BARABAR
KUU YA KONDOA-BABATI.
AMESEMA LORI HILO AINA YA ISUZU LENYE NAMBA T800 AJF LIKUWA LIMEPAKIA
WATU 87 AMBALO LILIKUWA LIKITOKEA BEREKO KUELEKEA PAHI WILAYANI
KONDOA.
ZELOTHE AMESEMA GARI HILO LILIPOFIKA KATIKA ENEO HILO AMBALO KUNA
MTEREMKO MKALI NA KONA LILIACHA NJIA NA KUGONGA MWAMBA HATUA
ILIYOFANYA KUPINDUKA MARA MBILI JAMBO LILILOFANYA WATU KUPOTEZA MAISHA
NA KUUMIA VIBAYA.
AIDHA AMESEMA KATIKA TUKIO HILO WATU 14 WALIPOTEZA MIASHA KUTOKANA NA
AJAHI HIYO AMBAPO WENGINE WALIFIA HOSPITALI WAKATI WAKIPATIWA
MATIBABU.
AMESEMA DEREVA WA GARI HILO MOHAMEDI RAJABU AMBAYE NDIO MMILIKI WA
GARI HILO AMETOKEWA BAADA YA TUKIO HILO HUKU JITIHADI ZA KUMTAFUTA
ZIKIENDELEA ILI AWEZE KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa