Home » » WASIMAMIZI WA MITIHANI DARASA LA SABA WAASWA KUTOVUJISHA MITIHANI‏

WASIMAMIZI WA MITIHANI DARASA LA SABA WAASWA KUTOVUJISHA MITIHANI‏


Masoud Masasi Katavi yetu Blog
WAKATI mitihani ya darasa la saba inanza sept 19 mwaka huu ambapo itafanyika kwa muda wa siku mbili nchini kote wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi umejipanga kuhakikisha mitihani hiyo haivuji kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Kuvunja kwa mitihani na masuala ya udanganyifu yaliyokuwa yakifanywa na wasimamamizi wa mitihani kwa kushirikiana na walimu wa shule husika yalileta mzozo mkubwa na kuifanya wizara ya elimu iwe kikaangoni.
Katika mkoa wa Dodoma rai imetolewa kwa Wasimamizi wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi katika Manispaa Dodoma ambapo wameaswa kutoruhusu masuala ya udanganyifu katika usimamizi wao.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw, Robert Kitimbo amesema Wasimamizi hao wameapishwa na hivyo wafanye kazi kwa mujibu wa kiapo chao.

Amesema katika kiapo chao wameapishwa ili watunze Siri hivyo wasimamie kutokanana maagizo waliyopewa katika semina ili kuepusha kuvunja sheria na uvujaji wa mitihani.


Kwa upande wa watahiniwa amewaasa kutoogopa mtihani na kuuona kuwa ni kitu tofauti na kuwataka kutoibia mtihani.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya mtihani huo ndugu Kitimbo amesema mitihani imehifadhiwa vizuri na inagawiwa leo na kwamba hakuna tatizo lolote lililojitokeza.


Akielezea kuhusu Imani yake katika ufaulu wa wanafunzi amesema Imani yake ni kuwa ufaulu utakuwa juu kwa asilimia 75 kutokana na maandalizi waliyoyafanya nakuongeza kuwa zaidi ya wanafunzi elfu 6 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumalizaElimu ya Msingi katika Manispaa hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa