Home » » WAZAZI WATAKIWA KUACHA KUOZA WATOTO WAO WANAPOMALIZA DRS 7‏

WAZAZI WATAKIWA KUACHA KUOZA WATOTO WAO WANAPOMALIZA DRS 7‏


Masoud Masasi,Dodoma
WAZAZI nchini wametakiwa kuachana na tabia za kuwaoza watoto wa kike  pindi  wanapomaliza elimu yao ya msingi kitendo ambacho kimekuwa kikiwanyima haki yao ya elimu kwa kuwakatisha masomo kwa madai ya kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha.
Ushauri ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maji na Maendeleo Mkoani Dodoma (MAMADO),Godwin Mkanwa wakati wa mahafali ya kumi ya Shule ya Msingi Lusinde iliyopo Wilayani Chamwino mkoani hapa.
Mkanwa alisema tabia ya wazazi kuwaoza watoto wa kike badala ya kuwawekea  mipango ya kuwaendeleza kielimu kwa manufaa ya baadae imekuwa ikishamili hapa nchini hasa katika maeneo ya vijijini.
Amewaagiza viongozi wa kata hiyo kuhakikisha wanalisimamia hilo na pamoja na kuhakikisha wanafunzi wote wa kike wanaomaliza elimu ya msingi wanaendelea na masomo yao kama ilivyo kwa watoto wa kiume.
Pia aliwataka wakuu wote wa Shule za Msingi zilizopo katika Wilaya hiyo ya Chamwino kuhakikisha maeneo ya shule zao yanapimwa na kufahamika vizuri mipaka yake kwa lengo la kuepuka migogoro ya ardhi ambayo inajitokeza katika maeneo mengi hapa nchini.
Mkanwa alisema  kuwa hivi sasa kumekuwepo na wavamizi wa maeneo jambo ambalo linasababisha kuzuka kwa migogoro isiyokuwa ya lazima.
Katika  hatua nyingine Mkwana alisema  shirika la MAMADO limekuwa likiisaidia shule hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo limeweza kutekeleza miradi yenye thamani ya shilingi milioni 35.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa