Home » » Mithani Darasa 7 yaendelea Dodoma‏

Mithani Darasa 7 yaendelea Dodoma‏


Na Masoud Masasi Dodoma
MITIHANI ya darasa la saba inayoendelea toka juzi ambapo mkoani hapa katika baadhi ya shule hali imekuwa ni shwari huku watahiniwa  wanaofanya mitihani hiyo wakisema wana uhakika wa asilimia mia ya kufanya vizuri kutokana na kujiandaa vilivyo.
Gazeti hili lilitembelea shule za Chamwino A na B,Uhuru,Kiwanja cha Ndege na Chinangali ambapo ilikuta hali shwari katika shule hizo huku wanafunzi hao wakiwa madarasani wakifanya mitihani hiyo.
Wakizungumza wakati wa mapumziko hayo watahiniwa hao walisema katika mitihani waliofanya mtihani wa hisabati ndio wana wasiwasi nao kutokana na mfumo wa  sasa wa kujibu maswali kuwachanganya.
“Huu mfumo wa mwaka huu katika kujibu maswali kwenye mtihani wa hisabati umetuchanganya sana nah ii utatufanya tuweze kufeli lakini mtihani haujakuwa mgumu sana tatizo jinsi ya kujibu maswali’’alisema  Hawa Huseini.
Walisema lakini wamejipanga vizuri  katika mitihani mingine inayofuatia kwa kuwa wamejiandaa vilivyo katika mitihani hiyo.
Mmoja wa wasimamizi wa mitihani hiyo katika shule ya msingi Chinangali ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema tokea kuanza kwa mitihani hiyo jana hali ni shwari hakuna tatizo lolote lililojitokeza katika mitihani hiyo kwenye shule hiyo.
Katika Manispaa ya Dodoma zaidi ya watahiniwa 6000 wanafanya mtihani huo wa kumaliza elimu yao ya msingi mkoani hapa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa