Home » » LSF:MCHAKATO WA SHERIA YA WATOA MSAADA WA SHERIA KUKAMILIKA MWISHONI MWA 2013‏

LSF:MCHAKATO WA SHERIA YA WATOA MSAADA WA SHERIA KUKAMILIKA MWISHONI MWA 2013‏


Masoud Masasi,Dodoma
MFUKO wa Wasaidizi wa Sheria(LSF)umesema hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2013 mchakato wa sheria ya watoa msaada wa sheria na sheria ya wasaidizi wa sheria nchini utakuwa imekamilika.
 Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Mfuko wa wasaidizi wa sheria (LSF) Kees Groenendijk wakati akifungua warsha ya wasaidizi wa sheria katika ukumbi wa Dodoma Hotel mjini hapa ambayo iliwakutanisha wasaidizi hao kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.
Groenendijk alisema hiyo ni hatua kubwa ambayo itawezesha wasaidizi hao kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi pamoja na  kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wengi ambao hawajui lolote kuhusiana na mambo ya kisheria hapa nchini.
 Alisema hivi sasa wapo kwenye mchakato wa  kutengenezwa kwa muswada wa sheria hiyo ambapo watapita kwa wasaidizi wa sheria na kukusanya maoni yao kwa ajili ya kuuboresha zaidi muswada huo.
 Aidha  meneja huyo wasaidizi  hao wanafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Mtandao wa Wasaidizi  wa Sheria Nchini (TAPANET) wana uwezo wa kuzifikia wilaya 50 hadi 60 hapa nchini ingawa kuna changamoto ya ongezeko la wilaya mpya kila siku.
“Ifikapo mwishoni mwa mwakani mchakato wa sheria ya watoa msaada wa sheria ya wasaidizi nchini utakuwa umekamilika na maandalizi yanaendelea kufanyika”alisema Groenendijk.
 Alisema wananchi wengi wanakabiliwa na changamoto ya kutojua sheria hivyo ni wajibu wa kila msaidizi wa sheria kufanya kazi yake ya kuelimisha umma katika kutoa msaada huo wa kisheria.
“Wananchi wengi hapa nchini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutojua sheria kabisa hvyo ni wajibu wa kila msaidizi wa sheria kufanya kazi ya kuwaelimisha umma”alisema
 Alibainisha kuwa  yapo mambo mengi ya kisheria yanayotakiwa kuwafikia wananchi na ambayo hawayajui kabisa ikiwemo masuala ya ardhi na mirathi ya ndoa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa