Home » » WAZAZI WA WATOTO VIZIWI WAOMBA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA‏

WAZAZI WA WATOTO VIZIWI WAOMBA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA‏


Na Masoud Masasi- Dodoma yetu Blog
WAZAZI na Walezi zaidi ya 20 wenye watoto wanaoishi na ulemavu wa
kutosikia wamesema mradi wa mafunzo ya lugha ya alama ya namba ya
kujifunza kwa mikono kwa herufi itakayowawezesha kupata mbinu namna ya
kuwasiliana kwa vitendo utaweza kuwasaidia wao kuweza kuwasiliana na watoto wao.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Chama cha Chavita Wilaya ya Kondoa
Ally Jumanne alipokuwa akizungumza kwenye mafunzo ya lugha ya alama
ya kujifunza kwa mikono herufi iliyowashirikisha wazazi na walezi
wanaoishi na watoto wenye ulemavu wa kutosikia kutoka vijiji vya Pahi
Wilaya ya Kondoa.
Jumanne alisema kwenye Kata hiyo kuna idadi kubwa ya watoto wenye
ulemavu wa kutosikia lakini changamoto iliyopo ni wazazi na walezi hao
kutofahamu jinsi ya mawasiliana kwa njia ya mikono kwa kutumia
alfabeti ambayo inayotumiwa na viziwi wote.
“Kwenye kata hii kwa kweli kuna watoto wengi wenye ulemavu wa
kutosikia na changamoto iliyopo ni wazazi na walezi kutofahamu jinsi
ya kuweza kuwasiliana nao kwa kutumia mikono na alfabeti”alisema
Jumanne.
Alisema mafunzo yaliyoandaliwa kwa ufadhiri wa shirika lisilo la
Kiserila la The Foundation for Civic Society, waliyoyapata wazazi na
walezi yatawawezesha kutumia njia nyepesi ya kuwasiliana na watoto wao
wenye ulemavu huo tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakishindwa
kuelewana wao kwa wao katika mawasiliano .
Hata hivyo alisema kuwa pamoja na mradi huyo wa mafunzo ya lugha ya
alama Wilaya ya Kondoa bado viziwi wengi wanaoishi vijijini
wamebainika kutumia lugha ya asili badala ya lugha ya Taifa
inayokubalika na karibu mataifa mengi.
Naye mwezeshaji wa mradi wa mafunzo wa lugha ya alama Wilaya ya Kondoa
Mariam Athumani,aliiomba serikali mashirika na taasisi mbalimbali
kukisaidia chama cha chavita Kondoa fedha ili kiweze kutoa elimu ya
lugha ya alama kwa watu wasioifahamu.
Mariam alisema Chama hicho kikifadhiriwa kitaweza kuwafikia viziwi
walio wengi ambao wanaoishi vijijini ambao hawajui namna ya
kuwasiliana kwa kutumia lugha ya alama inayotumika ya Kitaifa.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa mafunzo ya lugha ya alama Wilaya
ya Kondoa Mustapha Shabani amewataka wazazi na walezi kuungana na
chama cha chavita kupinga usemi unaotumiwa wa kuwaita viziwi kwa jina
la mabubu.
Alisema viziwi wana mawasiliano yanayoweza kuwasiliana na mtu yoyote
hivyo hakuna sababu ya kuwaita watu hao mabubu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa