Masoud Masasi,Dodoma yetu BlogCHAMA cha mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma(Dorefa)kimesema kuwa kimebainimoja ya migogoro inayojitokeza mkoani hapa inasababishwa na viongozina mashabiki wa soka kutokujua kabisa sheria za soka na kanuni zamashindano hatua waliyosema ndio imekuwa chanzo cha migogorombalimbali.Hayo yalibainishwa na Mwenyekit wa Dorefa Nasoro kipenzi alipokuwaakizungumza i juu ya migogoro mbalimbali ambayo imekuwaikijitokeza katika mashindano mbalimbali mkoani hapa.Ibrahim alisema kuwa viongozi wengi wa vilabu vya soka pamoja namashabiki wamekuwa hawajui kwa kiasi kikubwa sheria za soka na kanuniza mashindano jambo linalofanya kuwepo kwa migogoro ambayo hailetitija kwa maendeleo ya soka la Dodoma.“Baadhi ya viongozi wa vilabu na wapenzi kutokufahamu vyema sheria zasoka na kanuni za mashindano na hivyo kuwa ni chanzo cha migogorombalimbali ambayo inatokana na wengi kutojua sheria na kanunihizo”alisema IbrahimKatibu huyo alisema chama hicho kimekuwa kikifanya semina elekezimbalimbali mkoani hapa kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi mbalimbalilengo likiwa ni kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhususheria na kanuni za mashindano ili kuepuka migogoro inayojitokeza."Tumekuwa tukifanya semina mbalimbali kwa vilabu vyetu vyote vya mkoawa Dodoma kila inapotokea mashindano mbalimbali na hii katika kusadiakupunguza migogoro hiyo kwani tatizo ni kutojua sheria na kanuni zamashindano na hii kidogo itasaidia"alisema katibu huyo
Home »
 » DOREFA YABAINI TATIZO LA MIGOGORO YA SOKA DODOMA
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment