Masoud Masasi,Dodoma
KATIKA kuhakikisha utendaji wa kazi wa waandishi wa habari unafanyika kwa ufanisi Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma(CPC)kitakopesha computer ndogo za mkononi(Laptop) saba kwa wanachama wake zenye thamani ya sh 3.5 milioni.
Hayo yalibainishwa juzi na Katibu mkuu wa CPC Habel Chidawali wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mjini hapa.
Chidawali alisema kwa kuanzia watakopesha computer saba ndogo zenye thamani y ash 3,500,000 kwa wanachama wake ambapo amesema kila mwanachama anayetaka kukopa anatakiwa kulipa sh 500,000 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Alisema mradi huo wa kukopesha computer hizo utadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo baada ya hapo wanachama wengine watakopeshwa tena baada ya wale wa mwanzo kumaliza mkopo huo.
“Hizi computer tutakopesha kwa wanachama wetu sina thamani ya sh 3,500,000 na kila mwanachama atakayechukuwa anatakiwa kulipa sh 500,000 kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja ili baada ya hapo na wengine waweze kuchukuwa mkopo huu na hakuna riba yoyote itakayotozwa”alisema Chidawali.
Katibu huyo alibainisha kuwa lengo la kutoa mkopo huo ni kuwajengea uwezo wanachama wake katika kufanikisha utendaji wao wa kazi wa kila siku ambapo amesema wanajipanga pia katika kipindi kijacho kuwaendeleza kielimu wanachama wake.
Alisema chama hicho kipo katika mikakati ya kuwa na miradi mbalimbali ambayo itakayowawezesha chama hicho kuwa na kipato cha uhakika ambacho kitaweza kuwasaidia wanachama wake katika shughuli mbalimbali ikiwepo kuwasomesha na kuwaongezea kipato katika kuwapatia mikopo mbalimbali.
Mratibu wa Chama hicho Daniel Msangya alisema kwa wale wanaotakiwa kukopesha computer hizo kuandika barua za maombi ambapo wametakiwa kueleza jinsi gani wataweza kulipa kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na kuahidi kutoa pesa ya asilimia kuanzia 10 ya mkopo huo.
0 comments:
Post a Comment