BAADHI ya wajasirimali wanawojishughurisha na uuzaji wa samaki wa kukaanga katika eneo la Bahi Sokoni wilayani hapa wamesema kinachochangia wao kuogopa kwenda kukopa kwenye taasisi za mikopo ni riba kubwa wanayokatwa pindi wanapochukuwa mikopo jambo linalowafanya kutochukuwa mikopo kwenye taasisi hizo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani hapa wajasirimali hao wamesema wanapoenda kuchukuwa mikopo katika taasisi za mikopo huwa wanakatwa riba kubwa hali inayochangia kufa kwa mitaji yao.
Wamesema wanapochukuwa mikopo fedha zote uishia kulipia marejesho kutokana na riba kuwa kubwa wanayokatwa na baadae hadi mtaji unakufa.
Joseph Sanga amesema hatua hiyo imewafanya wao kuogopa kwenda kuchukuwa mikopo kwenye taasisi hizo kuhofia kukatwa riba kubwa hali inayofanya kufanya biashara kwa mitaji midogo kwa kuhofia kwenda kukopa.
Haruna Idrissa amesema licha ya riba kuwa kubwa pia mkopo unaopewa ni mdogo kwani ukitaka mkopo mkubwa lazima masharti yake ni makubwa sana kitu ambacho akiwezi kuongeza mtaji wako na badala yake ndio unaua mtaji.
Wamesema hali hiyo inawalazimu kwenda kukopa samaki hao kwa mali kauli kwa wachuuzi wa samaki hao hatua inayofanya kuwa na mtaji mdogo wa biashara hiyo.
Wajasiriamali hao waliiomba serikali kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha waliyokuwa nayo kutokana na wao kuwa na majukumu ya kifamilia.
Wananchi wa wilaya ya Bahi wamekuwa wakijishighulisha na kazi mbalimbali katika kujipatia kipato cha kila siku pamoja na familia zao kitu ambacho kama wakiwezeshwa wanaweza kufika mbali.

0 comments:
Post a Comment