Masoud Masasi,Dodoma
LIGI taifa ngazi ya Wilaya ya Dodoma mjini inatarajiwa kutimua vumbi Octoba 6 mwaka huu katika viwanja viwili tofauti ambapo timu 20 zitachuana kutamfuta bingwa wa wilaya hiyo.
Akizungumza na Mwananchi katibu msaidizi wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Dodoma Mjini(DUFA)Said Mohamed Babuji alisema jumla ya timu 20 zitashiriki ligi hiyo ambapo amesema kutakuwa na makundi mawili.
Babuji alisema kila kundi lina timu 10 na kila kundi litatoa timu tatu za juu ambapo itachezwa hatua ya sita bora ambayo bingwa wa Wilayaatawakilisha wilaya kwenye ligi ya Mkoa pamoja na mshindi wa pili na watatu.
Alizitaja timu hizo kuwa ni Dodoma Sports,Kisasa Fc,Gwasa United,Nungu Fc,Saratoga,Ac Hungry,Area C,Cardif Fc na West Chinangali huku kundi B ni timu za Dundee United,Jupiter,KBC,Area D,Kikuyu Fc,Vijana Stars, Hazina,Pentagon,Area A na Ipagala Fc.
Katibu huyo alisema ligi hiyo itaanza kuchezwa Octoba 6 kwenye viwanja vya Jamhuri Sekondari na Central Sekondari ambapo amesema timu ya Kisasa na Gwassa itacheza katika ufunguzi wa ligi hiyo.
Alisema msimu huu wa ligi hiyo hawatakuwa na huruma kwatimu ambazo zitaonyesha utovu wa nidhamu ambapo amesema hawatasita kuzichukulia hatua kali za kisheria .
0 comments:
Post a Comment