Masoud Masasi,Dodoma
UONGOZI mpya wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoani Dodoma(DOREFA)imeunda kamati nne ikiwemo yaIdara ya habari na Uenezi ili kuweza kukiendesha chama hicho katika shughuli mbalimbali.
Akizungumza na Mwananchi Katibu wa DOREFA Stewart Masima alisema kamati hizo zimeundwa kwa ajili ya kuweza kukimarisha chama hicho katika utendaji wake wa kazi ambapo amesema kamati hizo zitadumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Masima alitaja kamati hizo kuwa ni Kamati ya Waamuzi,Uchaguzi,fedha na Idara ya Habari na uenezi ya chama hicho.
Katibu huyo alibainisha kuwa lengo la kuingiza kamati mpya ya idara ya habari na uenezi ni kutambua mchango mkubwa wa waandishi wa habari za michezo mkoani Dodoma hivyo wakaamua kuwepo kwa kamati hiyo itakayowapatia taarifa mbalimbali za chama hicho.
“Safari hii DOREFA tumeongeza kamati ya Habari na Uenezi hii tumeongeza kwa sababu ya kutambua mchango wa waandishi wa habari mkoani hapa hivyo sasa wataweza kupata habari kwa uwazi mkubwa kupitia kamati hii ’’alisema Masima.
Kamati hiyo inaundwa na Fatma Gaffus,Pendo Mtibuche,Masoud Masasi,Sifa Lubasi,Ramadhani Masaibu,Nuru Mkupa na Kepher Maswaga.
0 comments:
Post a Comment