Na Masoud Masasi
SERIKALI imetakiwa kuunda sera ya uzalishaji wa mafuta ya kula itakayo saidia kuwepo kwa ushindaji wa haki kwa wasindikaji wa ndani na nje ya nchi ambapo imeelezwa itaweza kusaidia kuwepo kwa ushindani wa soko hilo.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wasindikaji wa Mafuta ya kupikia Kanda ya Kati (Cezosopa) Ringo Iringo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa kuhusu uzalishaji na soko la mafuta hayo hapa nchini.
Iringo amesema kuwa kutokuwepo kwa sera ya mafuta nchini ndio kumekuwa kukichangia kutokuwepo kwa ushindani wa haki kwa wazalishaji wa mafuta wa ndani na nje wanaoingiza mafuta yao nchini bila kuwepo kwa kiwango maalumu.
Amesema kuwa umefika wakati sasa serikali kuunda sera hiyo ambayo itawawezesha wasindikaji wa ndani kuweza kuzalisha mafuta kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyo sasa.
Alibainisha kuwa hivi sasa Tanzania inazalisha asilimia 40 ya mafuta hayo wakati yanayo agizwa kutoka nje ya nchi ni asilimia 60 kiwango ambacho kinawakatisha tamaa wazalishaji wengi hapa nchini.
Suala la uingizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi limekuwa likipigiwa kelele na wazalishaji wa mafuta hayo hapa nchini kutokana na kuuzwa bei ya chini huku yanayozalishwa hapa nchini yakiwa juu kutokana na viwango kudaiwa kutofautiana
0 comments:
Post a Comment