Na Dodoma yetu Blog
WENYEVITI wa vitongoji wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamefanya maandamano kwenda katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kudai posho zao walizoahidiwa kupatiawa kutokana na kushiriki katika kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kitongoji cha Salama wilayani hapo Samwel Maganjila, amesema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo kutokana na kuzungushwa kwa muda mrefu kuapatia stahili zao.
Maganjila amesema kuwa kutokana na taarifa mbalimbali zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kila mwenyekiti wa kitongoji alitakiwa kulipwa kiasi cha sh. 35,000 kwa siku zote saba za zoezi hilo lakini hali imekuwa tofauti kwakuwa wamekuwa wakipigwa danadana katika suala la malipo.
Amebainisha kuwa pana kufanya maandamano hayo kwenda kwa mkuu huyo wa wilaya baadhi yaoa wamepatia sh, 8,000 na wngine sh. 24,000 kiasi ambacho wamekipokea kwakuwa wameahidiwa kuwa pesa zao kisha ingizwa wataitwa na kupatiwa mara moja.
Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya hiyo Fatuma Saidi, amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa tayari limeshafanyiwa kazi kwa kuwalipa pesa zao wakuu wavitongoji hao.
Saidi amesema wenyeviti hao watapatiwa pesa hizo hivi karibuni kutokana na mchakato wa malipo yao umeshakamilika.
0 comments:
Post a Comment