Home » » MKAZI WA DODOMA AJINYONGA NA KUACHA UJUMBE BAADA YA KUHISI KUMUUA MCHUMBA WAKE.

MKAZI WA DODOMA AJINYONGA NA KUACHA UJUMBE BAADA YA KUHISI KUMUUA MCHUMBA WAKE.

Ujumbe Wenyewe ndio Huu. 
Na Nathaniel Limu.
Ujumbe ulioachwa na Oscar John (24) mkazi wa mkoa wa Dodoma  aliyejinyonga hadi kufa baada ya kuhisi amemuuwa mchumba wake kwa kumkata kata kwa kisu,umepatikana.
Oscar alijinyonga chumbani kwa mchumba wake Maria Chilinde (25) ambaye ni mfanyakazi wa chuo cha VETA mjini Singida baada ya kumkata kata kwa kutumia kisu.
Katika ujumbe huo, marehemu Oscar aliandika  ‘mimi Oscar John nimekufa pamoja na Maria,hela elfu tisini pamoja na simu zangu watachukua wazazi wangu.By by wapendwa wote’.
Kwa mujibu wa mkuu wa chuo cha VETA mjini Singida Afridon Mukhomoi, marehemu Oscar atakuwa ameandika ujumbe huo baada ya kubaini amemuuwa Maria na alipomaliza kuuandika, alijitundika kwenye kenchi kwa kutumia pazia na kusababisha kifo chake.
Amesema kuwa wakati tukio hilo la kusikitisha linatokea, yeye hakuwepo lakini alielezwa kuwa baada ya Maria kuzirai na Oscar kuhisi kuwa amefariki dunia, alimfunika kwa shuka na kuandika ujumbe huo na
Marehemu Oscar inadaiwa amefanya unyama huo baada ya wazazi wa Maria kudai mahari ya shilingi milioni mbili,ndipo aolewe na Oscar.Oscar alishindwa kumudu kiwango hicho na hivyo kuamua wote wafe. 

1 comments:

Anonymous said...

Ufinyu wa fikra ndo unao tupelekea kua na maamuz mabaya

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa