Mkurugenzi
wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa,Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma Bw.Charles Magaya akiongea kuhusu maadhimisho ya
Mwalimu Nyerere wakati wa kikao kazi kilichofanyika mjini Dodoma mapema
leo.Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Bw.Athanas Kolokota na Mkurugenzi
Msaidizi Thomas Manyambula (kushoto).
Na
Happiness Shayo-Utumishi
Maadhimisho ya kumuenzi Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanatarajiwa kufanyika kitaifa kesho
katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Hayo yalisewa na Mkurugenzi
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Bw.Charles Magaya alipokuwa katika kikao kazi cha maandalizi ya siku
hiyo mjini Dodoma.
Bw.Magaya alisema Siku ya
kumuenzi Baba wa Taifa itaongozwa na mmoja wa washiriki wa Baba wa Taifa Balozi
Job Lusinde. “Maadhimisho hayo
yataongozwa na mmoja wa washiriki wa Baba wa Taifa katika kupigania Uhuru wa
Tanganyika Mheshimiwa Balozi Lusinde ambaye pia ni muasisi wa Chama cha
TANU”alisema Bw.Magaya.
Sambamba na maadhimisho
hayo Bw.Magaya alisema kuwa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma
imeandaa sinema mbalimbali za Mwalimu Nyerere zitakazoonyeshwa katika viwanja
vya Nyerere Square leo kuanzia saa 12 jioni hadi saa 3 usiku. Aidha,aliwataka wananchi wa
mkoa wa Dodoma kushiriki katika maadhimisho hayo ya kumuenzi Baba wa Taifa.
Pia Bw.Magaya alitoa wito
kwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye
viwanja vya Nyerere Square ili kusikiliza hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi
waliofanya kazi karibu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Maadhimisho ya Baba wa
Taifa hufanyika Oktoba 14 ya kila mwaka ambapo mada mbalimbali hutolewa na
viongozi waasisi wa Taifa la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment