ZAIDI ya sh bilioni 20.8 zinatarajiwa kutumika kwa
ajili ya kuanzisha mradi wa kilimo cha mahindi na ufugaji wa kuku wa kienyeji
kwa wananchi waishio vijijini.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Meneja wa
mradi huo, Hem Chandro Roy, wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili.
Alisema mradi huo ambao unafadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Serikali ya Uingereza (DFID) na kuendeshwa kwa kushirikiana na
BRAC Tanzania, unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka minne ambapo
utawanufaisha wananchi kutoka mikoa 15 nchini.
Alitaja mikoa itakayonufaika na mradi huo kuwa ni
pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha,
Manyara, Singida, Tabora, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza, Shinyanga na Mara.
Alisema lengo la kuanzisha mradi huu ni kuwawezesha
wakulima na wafugaji wadogo waishio vijijini waweze kujikwamua kiuchumi na
kuondokana na umaskini.
Alifafanunua kuwa watasaidia kuboresha njia za
kulifikia soko, kuboresha njia za kufikia huduma za fedha na kuamsha na
kuhamasisha sekta binafsi ili kuwekeza katika kuongeza thamani na mlolongo wa
mazao.
Alisema jumla ya wananchi 105,000 watanufaika na
mradi huo huku Watanzania 104 wakipata ajira.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment