MKUU wa Wilaya
ya Mpwapwa, Christopher Kangoye, amewapa mwezi mmoja wakata mkaa wa wilayani
humo kuhakikisha wanajiunga kwenye vikundi maalum, kinyume na hapo
atawachukulia hatua kali za kisheria.
Kangoye alitoa agizo hilo jana, wilayani Mpwapwa, wakati alipokuwa akifungua mdahalo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa jamii, ambao uliandaliwa na Mitandao ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya wilaya hiyo.
Alisema ni vyema kwa wakazi ambao wanajihusisha na shughui za uuzaji mkaa kuhakikisha wanajiunga katika vikundi maalum ili waweze kutambulika na Maliasili kwa lengo la kutunza mazingira.
“Ni lazima wafanyabiashara hawa wa mkaa wakajiunga kwenye vikundi ambavyo vitakuwa rasmi ambapo wataweza kupewa vibali na Maliasili, ikiwemo maofisa misitu kuwasaidia kuwapa utaratibu wa upandaji miti na uvunaji miti kitaalamu, ili kuwa na mkaa wenye tija kwa lengo la kuweza kudhibiti uharibifu wa Mazingira,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini, George Foime, alisema wao kama Halmashauri tayari wameshatunga Sheria ndogo dhidi ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya hiyo.
Alisema sheria hiyo, inahusu faini kwa mwananchi ambaye atabainika kuchoma moto misitu atatozwa kiasi cha Sh 250,000.

Chanzo: Rai
0 comments:
Post a Comment