Home » » HAWA NI BAADHI YA WASANII WATAKAOTAMSHA LA KRISMAS MKOANI DODOMA KUFANYIKA UWANJA WA JAMHURI

HAWA NI BAADHI YA WASANII WATAKAOTAMSHA LA KRISMAS MKOANI DODOMA KUFANYIKA UWANJA WA JAMHURI

 
 Mwimbaji wa nyimbo za injili aliyeamua kuokoka akitokea kwenye mziki wa kizazi kipya aliibuka mwaka mwaka 2011 tokea Bongo Star Seach [BSS] Beatrice Williamu atatumbuiza kwanye tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja wa jamuhuri Dodoma.
Tumsifu Rufutu Tokea nchini Kenya atatumbuiza kwenye tamasha hilo kwa kuwaongoza watu kwenda kaananina albamu yake ya Mwambie Farao ndani ya viwanja hivyo vya jamuhuri Dodoma.

Na Mwandishi wetu ,Dodoma
TUMSIFU Rufutu kutoka nchini Kenya aliyeimba na albam yake iliyobebwa na wimbo wa Mwambie Farao anatarajia kukonga nyoyo za wanadodoma katika Tamasha la krismas litakalofanyika Des 25 mwaka huu.
Tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja wa jamuhuri mjini Dodoma linatarajia kuwa kivutio kwa wananchi wa mkoa huo kutokana na kuwahusisha waimbaji wa nyimbo za injli wenye vipaji vya hali ya Rufutu alisema amejiandaa vya kutosha ili kukonga nyoyo za wapenzi wa nyimbo za injili kutokana na yeye kuwa na hamu kubwa ya kufanya hivyo huku akifikisha ujumbe wa uhakika wa neno la Mungu.
Aliwataka wapenzi hao kujiandaa vya kutosha kwani siku hiyo ya kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu itakuwa ni siku pekee kwao kwani atawaongoza kumsifu Mungu kwa vitendo vya uhalisia kupitia ngoma, filimbi na vinubi. ‘’wapenzi wangu waliopo Dodoma pamoja na mikoa jirani wafike kwa wingi huku wakitarajia kumuona Nabii Mussa mzee wa mwambie Farao wimbo waje na Viti, Meza na vitu vingine walivyo navyo ili tuelekee kaanani pamoja kuteka Baraka’’, alisema
Pamoja na msanii huyo Tokea nchi jirani ya Kenya atakaewaongoza watu kuelekea kaanani ataambatana na waimbaji wengine wa hapa nchini tokea jijini Dar es saalam akiwemo Beatrice William aliyeanzia Bongo Star
Sech na kuamua kuokoka na kujikita kwenye nyimbo za injili huku akitamba na wimbo wa akina Delila wapo. Waimbaji wengine ni pamoja na Sospeter Jonas Mzungu mzee wa Mshumaa na Marry Sinkala wote toka jijini watakasindikizwa na waimbaji mbalimbali wa mkoa huo ambao kwa pamoja watakuwa wakilitawala Jukwaa na kuwaongoza wapenzi wao kwa kumsifu Mungu ipasavyo.
Kwa upande wa waandaji wa Tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja wa jamuhuri, Liberty Promotion Company kupitia kwa msemaji wake mkuu John Banda alisema wamejiandaa vizuri kukonga nyoyo za wanadodoma kwa kuwawekea kiingilio cha 2000 kwa 1000 tu ili watu wengi wapate kushiriki.
Banda Alisema lengo la tamasha hilo ni pamoja na kuwachangia watoto yatima, wasiojiweza na katika mazingira magumu kutokana na sehemu ya mapato yatakayopatikana ili kuwawezesha vijana kuifanya Tanzania Bora.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa