Home » » Mbunge atokwa machozi

Mbunge atokwa machozi



MBUNGE wa Viti Maalumu, MaryStella Mallac (CHADEMA), alitokwa machozi baada ya kusimuliwa mkasa wa mwanamke kubakwa na askari wakati wa operesheni ya kuwahamisha wananchi waliodaiwa kuingia eneo la hifadhi.
Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na baadhi ya polisi wa mkoa wa Mpanda ni cha kinyama na kinapaswa kulaaniwa na kila mtu.
“Nilishtushwa sana na taarifa za askari pamoja na askari wa wanyamapori kuwavamia wananchi hao na kuwachomea nyumba lakini kibaya zaidi ni kuanza kuwabaka kina mama.
“Suala hili nimelifikisha kwa RPC wa Katavi lakini hadi sasa ni mwezi mmoja hakuna kinachoendelea na mwanamke aliyebakwa anadai lifanyike gwaride la utambuzi lakini hata hivyo halijafanyika,” alisema Mallac.
Hata hivyo alisema kuwa siyo kweli kuwa wananchi hao wako katika eneo ya hifadhi kwani hata ramani inaonyesha kuwa walipo ni nje ya mipaka ya hifadhi ikiwa na muhuri wa halmashauri.
Alipotafutwa mkuu wa polisi mkoa wa Mpanda Dhahiri Kidavasheri simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila majibu.

Chanzo;Tanzani Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa