Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
Akizungumza jana na NIPASHE, Afisa Elimu mkoani Dodoma, Juma Kaponda, alisema amezuia wanafunzi wote wasifanye mtihani kwa sababu hiyo na pia usajili wao ni wa kughushi.
Alibainisha kuwa tangu mwaka 2010 shule ya kulio haikuwa na wanafunzi, hivyo waliopo ni wa mwaka huu ambao wanatambulika ni wa kidato cha kwanza.
“Tangu 2010 haikuwa na wanafunzi ambao kwa sasa wangekuwa form four (kidato cha nne), hivyo 2010, 2011, 2012 hakukuwa na wanafunzi... mwaka huu 2013 ndio imefanikiwa kupata wanafunzi 15 tu wa kidato cha kwanza,” alisema.
Aidha alifafanua kuwa wanafunzi hao 15 ndio wanaotarajiwa kufanya mtihani mwaka 2016 iwapo watafanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili 2014.
Alisema usajili wa hao watahiniwa ulikuwa wa kugushi kwani wamesajiliwa watu wa mtaani kwenda kufanya mtihani huo.
“Kama tangu 2010 ilikuwa haina wanafunzi na wala siyo wa kujitegemea sasa hao 32 ni wa wapi na aliyefanya hizi vurugu alishaondoka na bado hatujambaini mpaka sasa alishaingia mitini,” alibainisha afisa huyo.
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya The Dream Senter iliyopo Manispaa ya Iringa Mkungo Omari (25), amefariki dunia baada ya kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila kwa madai ya kuhofia kufanya vibaya mtihani wake wa kumaliza elimu ya sekondari ulioanza jana nchini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:45 usiku na kuwa chanzo cha ni kuhofia kufeli mtihani.
”Mwanafunzi huyo aliacha ujumbe wa barua chumbani kwake na kusema kuwa kifo hicho hakihusiki na mtu yeyote wala hana kisa na mtu yeyote bali ameamua kufa kutokana na kuhofia kufeli tena mtihani huo,” alisema.
Akizungumza na NIPASHE, shangazi wa marehemu huyo, Betha Nzugu, alisema juzi mwanafunzi huyo alikuwa akisoma na wenzake, lakini jioni majira ya saa 3:30 usiku kaka yake alikuta barua hiyo na simu yake mezani ndipo alipomuita shangazi yake na kumpa barua hiyo ili aisome na alipoisoma kichwa cha habari kiliandikwa “buriani kamwe hamtanikuta tena duniani”.
Jijini Dar es Salaam, mtihani huo jana ulifanyika katika mazingira ya amani na utulivu.
Baadhi ya shule ambazo gazeti hili lilizitembelea ni Jangwani.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Geradine Mwanisenga, alisema mitihani ilifika saa 11:45 alfajiri na ilianza saa 2:00 asubuhi.
Nyingine ni Azania ambayo mmoja wa wanafunzi wake, alisema baada ya kumaliza mtihani wa kwanza kuwa, kulikuwa na mikondo nane ya wanafunzi ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo.
Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Hananasif, , ambaye alikataa kutaja jina lake kwa madai kwamba siyo msemaji, alisema jumla ya wanafunzi 260 katika mikondo saba walifanya mtihani huo katika mazingira ya utulivu.
Wanafunzi Nasma Joho na Mahamoud Kauly, walisema mtihani huo wa kwanza wa Jigrafia, ulikuwa wa kawaida, lakini hawajajua ni sababu zilizomfanya mwenzao mmoja asiufanye.
Shule nyingine ni Benjamini Mkapa, ambayo mlinzi wake alisema, bosi wake alimwagiza kutowaruhusu waandishi wa habari kuingia ndani kwa kuwa wengine tayari walishafika shuleni hapo.
Watahiniwa waliojiandikisha kufanya mtihani huo ni 427,906, kati yao 367,399 watahiniwa wa shule na 60,507 wa kujitegemea.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment