Home » » Ataka serikali iwekeze kwenye elimu

Ataka serikali iwekeze kwenye elimu

MKUU wa Wilaya ya Kongwa, Alfred Msovella, ameitaka serikali kuwekeza zaidi katika elimu ili kupata wananchi wenye weledi wa kutosha.
Msovella alisema ili nchi iendelee lazima iwekeze katika elimu kwa asilimia kubwa ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na wahitimu 155 wa Chuo Kikuu Huria mkoani Dodoma waliotunukiwa vyeti vya ngazi mbalimbali.
Alisema kwa sasa vipo vyuo vikuu vingi hapa nchini na Kenya ambapo wanafunzi wa vyuo hivyo wanapatiwa mikopo na Serikali ya Tanzania licha ya kuwa vyuo hivyo si mali ya serikali.
Alisema kama hapatakuwepo na uangalifu wa kuboresha elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu ni wazi nchi za jirani kama Kenya na Uganda wataweza kuteka soka la ajira na Watanzania watabaki kulalamika kwa kukosa ajira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria Mkoa wa Dodoma, Maulid Maulid, alisema kwa sasa chuo hicho kinakabiliwa na miundombinu ya kufundishia.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa