Home » » Bunge laanza Dodoma leo

Bunge laanza Dodoma leo

BUNGE leo linaanza mkutano wa 14 huku likitarajiwa kujadili miswada iliyoachwa katika mkutano wa 13 ukiwamo wa Kura za Maoni. Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema jana kuwa mkutano huo wa 14 utakuwa wa wiki tatu na baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni a miswada iliyoachwa katika mkutano uliopita.


Aliitaja baadhi ya miswada hiyo kuwa ni Muswada wa Kura za Maoni na Muswada wa Takwimu.

Joel alisema kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kuanza leo asubuhi kwa kipindi cha maswali na majibu na baada ya hapo kitaahirishwa hadi kesho kupisha kamati mbalimbali ikiwamo ya uongozi kukutana kupanga ratiba.

“Baada ya kipindi cha mswali na majibu hakutakuwa na shughuli yoyote ya bunge na hivyo wabunge wote watahitajika katika kikao cha pamoja na kupata utaratibu wa bunge ,” alisema

Alisema hadi jana mchana ratiba kamili ya mkutano huo ilikuwa haijatoka kwa vile kamati ya uongozi ilikuwa haijakaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutawanyika kwa kamati kwa shughuli mbalimbali zilizopangiwa.

Kutokana marekebisho ya kanuni na utaratibu wa kutunga sheria za fedha na ununuzi, Bunge litatumia mkutano huu kupitia taarifa mbalimbali za kamati.

Awali taarifa hizo za kamati zilikuwa zikipitiwa wakati wa kikao cha bajeti lakini sasa zinapitiwa mapema kabla ya kikao hicho.

Chanzo;Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa