Mkaguzi Msaidizi wa Polisi IVONIA akitoa elimu ya usalama barabarani kwa watoto hao.
Baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali wawakilishi toka Jeshi la Polisi walipata chakula mchna na watoto hao waishio katika mazingira magumu.
Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma akikabidhi vifaa mbalimbali kwa Sista ANITHA KASANGA ambaye ni mlezi wa watoto hao.
Kamishna msaidizi wa polisi SUZAN KAGANDA akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Miyuji - URSOLINE SISTERS.
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma limetembelea kituo cha matumaini cha kulelea
watoto wanaoishi katika mazingira magumu URSOLINE SISTERS Kilichopo eneo
la Miyuji Manispaa ya Dodoma na kutoa msaada wa vitu mbalimbali
ikiwemo Mchele Kg. 50, Maharage Kg. 50, Sabuni Boksi 2, Mafuta ya
kupikia Lt. 20, Pamoja na chumvi.
Akiongea
na watoto hao katika kituo hicho Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
SUZAN KAGANDA – ACP amesema pamoja na jukumu la ulinzi na usalama wa
watu na mali zao, lakini pia ni jukumu la Polisi kuwatembelea watoto
hao wanaoishi katika mazingira magumu,pamoja na kutoa elimu ya usalama
wetu kwanza na usalama barabarani kwa kuongea nao na kuwaelekeza
majukumu ya ulinzi na usalama.
Kamishna
msaidizi wa Polisi KAGANDA aliwapongeza watoto wanne ambao wamefaulu
Darasa la saba kwa kuwapatia zawadi za Madaftari 36, Mikebe 4, Peni na
Penseli Boksi 4 na kusema kuwa wameonyesha moyo kwa walezi wao katika
kituo hicho.
Kwa
upande wake Sista ANITHA KASANGA kwa niaba ya masista wenzake ambao
wanajukumu la kuwalea watoto hao amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dodoma kwa kuthamini kazi inayofanywa na kituo hicho na kuwaunga mkono
kwa kutoa msaada kwa watoto hao na kuonyesha moyo wa ukarimu.
Aidha
Sista KASANGA alisema kituo hiki kipo chini ya Kanisa katoliki na
kilianzishwa mwaka 1995 kikiwa na jumla ya watoto 6 ambapo mpaka leo hii
kina jumla ya watoto 53, kwa hapa nchini Tanzania makao makuu ya kituo
yapo Mkoani Singida, lakini makoa makuu yake yanapatikana nchini Poland
na mpaka sasa kituo hiki kina jumla ya matawi 27 hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment