Home » » Washtushwa na uharibifu wa mazingira

Washtushwa na uharibifu wa mazingira

Dodoma. Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali mkoani Dodoma wamesema uharibifu wa mazingira nchini unaongezeka kwa kasi hivyo ni wakati wa Serikali na taasisi za dini kushirikiana kukabiliana na janga hilo.
Kwa misingi hiyo, wameitaka Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), kuwashirikisha viongozi wa dini zote nchini na kila mmoja atambue kuwa hilo ni tatizo linalohitaji mapambano shirikishi.
Akizungumza katika kikao cha siku moja kilichowajumuisha viongozi wa dini zote nchini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Stephen Munga alisema Serikali imewatenga viongozi wa dini wakati wao pia wana nafasi kubwa katika jamii.
Alisema suala la kukabiliana na uharibifu huo ni pigo kwa watu wote hivyo ni vyema Serikali ikawashirikisha.
Chanzo;mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa